SABABU 20 KWANINI HAUNA
PESA
1. Hauweki bajeti. Ni muhimu kupanga matumizi yako ya
kila siku/mwezi ilikuhakikisha pesa zako zinaenda kwenye mambo ya msingi tu.
2. Unafuata mkumbo. Ukiwa mwepesi kufanya yote ambayo
wenzako wanafanya utapata changamoto za kipato.
3. Hauwezi kusema ‘HAPANA’. Ukiwa mzito wa kukataa mambo ambayo
hayana tija kwenye maisha yako binafsi haswa kwenye masuala ya pesa basi utapata
changamoto za pesa siku zote.
4. Unadhani Serikali itatatua matatizo
yako yote. Sasa hii
ni changamoto kwa wengi. Unaweza kukuta tangu Rais Mwinyi ameingia madarakani
umekuwa ukilalamikia mambo yale yale..
5.
Unapenda kulaumu wengine. Maisha yako yapo kwenye himaya yako
na sio ya mtu mwingine yoyote
6.
Unadhani matajiri wote ni watu
wabaya. Unahusisha
utajiri na mambo mabaya.
7. Sikukuu zote zinaendana na zawadi. Sio kila sikukuu upeleke zawadi kwa
kila mtu kwenye mtaa wako.
8. Umeacha kujifunza. Msomaji wangu mpenzi, sababu unasoma
makala yangu hii basi unaweza ukaendelea kwenye point inayofuata maana wewe ni
mtu unayependa kujifunza.
9. Una tabia mbaya. Wote tuna tabia mbaya fulani, tabia
zingine zinagharimu pesa nyingi. Ni muhimu kuzitambua na kuziacha.
10.
Unanunua vitu hovyo hovyo. Unaweza ukarekebisha hii kwa kuweka
list ya vitu vya kununua ndani ya siku 30 na usinunue chochote nje yah ii list.
11.
Unacheza michezo ya kubashiri. Tatu mzuka, Biko na Sports Betting
imekuwa michezo yako ukitegemea kupata utajiri.
12.
Hauna malengo. Malengo ni jambo la msingi kweye
maisha. Kutokuwa na malengo ni sawa na kutembea kwenye giza totoro.
13.
Una marafiki wabaya. Marafiki wako wana mchango mkubwa
kwenye mafanikio yako. Kama hauna mafanikio, badilisha marafiki wako. Hapa
simaanishi uvunje wahusiano bali namaanisha utumie muda wako mwingi na watu
wanakusukuma kwenda kwenye malengo yako.
14.
Wewe ni mvivu. Hakuna namna, wote tunahitaji kuwa
na bidii ya kazi ili kutengeneza kipato cha kutosha na kufikia malengo.
15.
Haujithamini. Je umewahi kuomba nyongeza ya
mshahara? Ni muhimu kujua thamani yako.
16.
Hauwekezi au kujilipa wewe kwanza. Kuwekeza na kuweka akiba ni muhimu
sana, usitumie pesa yote unayoitengeneza.
17. Haulipi zaka. Haujalishi wewe ni dini gani ila ni
muhimu kurudisha shukrani kwa muumba wako mwenye kukuwezesha kwenye yote.
18.
Haupitwi na sherehe yoyote. Kila mwezi unahudhuria harusi sio
chini ya tatu, unachanga kwenye sendoff, kitchen party na harusi yennyewe. Hapo
bado mavazi.
19.
Haujui pesa zako zinaenda wapi. Unatumia pesa bila kujua zinaenda
wapi. Ni muhimu kujua kila senti unayiotenegeneza inaenda wapi. Tumia
application za simu kama Expenses Manager kujua matumizi yako.
20.
Unadharau biashara za aina fulani. Majivuno yanakuzuia kufanya biashara
za aina fulani ambazo zina uwezo wa kukuongezea kipato.
Tuambie
ngapi kati ya hizi zinakuhusu na unafanya nini ili kukabiliana na tabia hizi
mbaya ambazo zinaumiza afya ya wallet yako.

