Wednesday, 21 November 2018

SABABU 20 KWANINI HAUNA PESA




SABABU 20 KWANINI HAUNA PESA

1.       Hauweki bajeti. Ni muhimu kupanga matumizi yako ya kila siku/mwezi ilikuhakikisha pesa zako zinaenda kwenye mambo ya msingi tu.

2.   Unafuata mkumbo. Ukiwa mwepesi kufanya yote ambayo wenzako wanafanya utapata changamoto za kipato.

3.       Hauwezi kusema ‘HAPANA’. Ukiwa mzito wa kukataa mambo ambayo hayana tija kwenye maisha yako binafsi haswa kwenye masuala ya pesa basi utapata changamoto za pesa siku zote.

4.          Unadhani Serikali itatatua matatizo yako yote. Sasa hii ni changamoto kwa wengi. Unaweza kukuta tangu Rais Mwinyi ameingia madarakani umekuwa ukilalamikia mambo yale yale..

5.           Unapenda kulaumu wengine. Maisha yako yapo kwenye himaya yako na sio ya mtu mwingine yoyote

6.           Unadhani matajiri wote ni watu wabaya. Unahusisha utajiri na mambo mabaya.

7.      Sikukuu zote zinaendana na zawadi. Sio kila sikukuu upeleke zawadi kwa kila mtu kwenye mtaa wako.

8.     Umeacha kujifunza. Msomaji wangu mpenzi, sababu unasoma makala yangu hii basi unaweza ukaendelea kwenye point inayofuata maana wewe ni mtu unayependa kujifunza.

9.       Una tabia mbaya. Wote tuna tabia mbaya fulani, tabia zingine zinagharimu pesa nyingi. Ni muhimu kuzitambua na kuziacha.

10.       Unanunua vitu hovyo hovyo. Unaweza ukarekebisha hii kwa kuweka list ya vitu vya kununua ndani ya siku 30 na usinunue chochote nje yah ii list.

11.       Unacheza michezo ya kubashiri. Tatu mzuka, Biko na Sports Betting imekuwa michezo yako ukitegemea kupata utajiri.

12.       Hauna malengo. Malengo ni jambo la msingi kweye maisha. Kutokuwa na malengo ni sawa na kutembea kwenye giza totoro.

13.       Una marafiki wabaya. Marafiki wako wana mchango mkubwa kwenye mafanikio yako. Kama hauna mafanikio, badilisha marafiki wako. Hapa simaanishi uvunje wahusiano bali namaanisha utumie muda wako mwingi na watu wanakusukuma kwenda kwenye malengo yako.

14.       Wewe ni mvivu. Hakuna namna, wote tunahitaji kuwa na bidii ya kazi ili kutengeneza kipato cha kutosha na kufikia malengo.

15.       Haujithamini. Je umewahi kuomba nyongeza ya mshahara? Ni muhimu kujua thamani yako.

16.       Hauwekezi au kujilipa wewe kwanza. Kuwekeza na kuweka akiba ni muhimu sana, usitumie pesa yote unayoitengeneza.

17.    Haulipi zaka. Haujalishi wewe ni dini gani ila ni muhimu kurudisha shukrani kwa muumba wako mwenye kukuwezesha kwenye yote.

18.       Haupitwi na sherehe yoyote. Kila mwezi unahudhuria harusi sio chini ya tatu, unachanga kwenye sendoff, kitchen party na harusi yennyewe. Hapo bado mavazi.

19.       Haujui pesa zako zinaenda wapi. Unatumia pesa bila kujua zinaenda wapi. Ni muhimu kujua kila senti unayiotenegeneza inaenda wapi. Tumia application za simu kama Expenses Manager kujua matumizi yako.

20.       Unadharau biashara za aina fulani. Majivuno yanakuzuia kufanya biashara za aina fulani ambazo zina uwezo wa kukuongezea kipato.

Tuambie ngapi kati ya hizi zinakuhusu na unafanya nini ili kukabiliana na tabia hizi mbaya ambazo zinaumiza afya ya wallet yako.